TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA


SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) Aprili 5 lilifanya mashindano ya mchujo na kupata mabondia watakao wakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kanda ya tatu Afrika yatakayofanyika uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) tarehe 18-22 Aprili 2023. Na kushirikisha nchi 14 wanachama wa kanda ya tatu.
Mchujo huo umefanyika katika ukumbi wa mazoezi wa timu ya ngumi ya JKT Mgulani. Jumla ya mabondia 22, ikiwa wanaume 16 na wanawake 6 ndio waliochagulia miongoni mwa mabondia 56 walikuwa katika maandalizi ya mashindano hayo.
Mabondia waliochaguliwa ni wale walionyesha uwezo mzuri kuwashinda wenzao kutoka katika kambi tatu tofauti zilizokuwa zikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo kutoka katika kambi za timu ya ngumi ya Ngome, timu ya ngumi ya Magereza na timu ya ngumi ya JKT Mgulani.
Kwa sasa mabondia waliochaguliwa watafanya mazoezi katika kituo kimoja JKT Mgulani.
Kamati ya BFT imechagua kituo hicho kutokana na kuwepo kwa miundo mbinu mizuri ya kuwezesha kufanya mazoezi ya ngumi kwa ufanisi kwa maandalizi ya mwisho na ya pamoja.
Nchi zitakazo shiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Somalia, DR Congo, Congo Brazzaville, Afrika ya kati, Gabon, Cameroon na Equatorial Guinea.
Orodha ya majina ya mabondia waliochagulia wanaume, wanawake, Makocha na kamati ya ufundi imeambatanishwa katika “nyongeza B” ya taarifa hii.
(Makore Mashaga). Katibu Mkuu (BFT)
Wajumbe wa BFT: Mr. Joseph M. Kato, Mr. Michael Changalawe, Mr. Mafuru Mafuru Mrs. Asha Voniatis, Mr. Ruger Kahwa, Mr. Idd Lugundama, Mr. Samwel Kapungu.
ORODHA YA MABONDIA WA KIUME WALIOCHAGULIWA TIMU YA TAIFA
Karim Juma - 
Minimume
Yohana Keneth - Fly
Abdalah Salum - 
Bantam
Hassan Waziri - 
Feather
Rashid Mrema - 
Light
Alex Isendi - 
Light Welterweight
Mohamed Swalahe - 
Light Welter
Atanas Ndiganya - 
Welter
Joseph Phillip - 
Light Middle
David Chanzi - 
Middle
Joshua Shadrack - 
Middle
Alphonce Abel - 
Middle
Yusuf Changalawe - 
Light Heavy
Nizza Abdalahamani - 
Light Heavy
Jofrey Peter - Cruser
Alex Sitta - 
Super Heavy
ORODHA YA MABONDIA WA KIKE WALIOCHAGULIWA TIMU YA TAIFA
Rahma - Minimum
Mariam Richard - 
Light Flyw
Shakila Abdalah - 
Fly
Aisha Iddi - 
Bantam
Leila Yazidu - 
Bantam
Beatrice Ambrose - Light
MAKOCHA
1. Samwel Batman – (IBA 1 Star)
2. Hassan Mzonge
3. Mussini Mohamed
4. Rogata Damian (IBA 1 Star)
5. Undule Lang’son
6. Haji Abdalah
KAMATI YA UFUNDI
1. Michael Changarawe – Mwanza
2. Robert Sululu – Dar es salaam.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post