CASEMIRO AING'ARISHA MAN UNITED, YASHINDA 1-0 UGENINI


BAO pekee la kiungo Mbrazil, Carlos Henrique Casimiro dakika ya tisa limeipa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality Jijini Bournemouth, Dorset.
Kwa ushindi huo, Manchester Unted inafikisha pointi 69, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 36, wakiwa mbele ya Liverpool yenye pointi 66 za mechi 37.
Kwa upande wao, Bournemouth baada ya adhabu ya leo wanabaki na pointi zao 39 za mechi 37 nafasi ya 14.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post