FAINALI EUROPA LEAGUE NI ROMA YA MOURINHO NA SEVILLA


TIMU ya AS Roma imefanikiwa kutinga Fainali ya Europa League baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Bayer Leverkusen kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu leo usiku wa Alhamisi Uwanja wa BayArena Jijini Leverkusen.
Timu hiyo ya kocha Mreno, José Mourinho inanufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Italia na sasa itakutana na Sevilla iliyoitoa Juventus.
Sevilla imeitoa Juventus kwa jumla ya mabao 3-2 kufuatia ushindi wa 2-1 jana Hispania ikitoka kutoa droo ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Italia.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post