MANCHESTER CITY WATWAA NA KOMBE LA FA, UNITED HOI


TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu, Manchester United jana Uwanja wa Wembley Jijini London.
Mabao ya Manchester City yalifungwa na kiungo Mjerumani, Ilkay Gundogan yote sekunde ya 12 ya dakika ya kwanza na 51, wakati bao pekee la Manchester United lilifungwa na kiungo Mreno, ' Bruno Fernandes dakika ya 33.
Hilo linakuwa taji la tatu msimu huu kwao baada ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post