SHEREHE ZA UBINGWA YANGA JUMAMOSI DAR ITAZIZIMA


SHEREHE za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara za Yanga zitafanyika Jumamosi kuanzia 3:00 asubuhi timu itakapokuwa inarejea kutoka Mbeya baada ya mchezo wake wa mwisho wa ligi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine.
Kikosi kitaondoka Mbeya mapema tu asubuhi baada ya mchezo wake na Prisons na kulakiwa na maelfu ya mashabiki wake huku wachezaji wakipanda kwenye gari maalum la kuonyesha Kombe lao.
Huu ni ubingwa wa pili mfululizo kwa Yanga na wa 29 jumla ambao unawafanya watanue rekodi yao ya kutwaa mara nyingi zaidi hadi mara saba zaidi ya watani, Simba.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post