TUISILA ROSSIEN KISINDA SI MCHEZAJI WA YANGA TENA


KLABU ya Yanga imetangaza kuachana na winga wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tuisila Rossien Kisinda baada ya nusu msimu wa kuwa na timu hiyo katika awamu yake ya pili.
Kisinda alirejea Yanga SC kwa mkopo dirisha dogo baada ya msimu mmoja na nusu wa kucheza RS Berkane ya Morocco.
Awali Mkongo huyo alijiunga na Yanga Agosti mwaka 2020 akitokea AS Vita ya kwao, Kinshasa kabla ya kutimkia Berkane Agosti 2021.
Anakuwa mchezaji wa pili kuondoka Yanga baada ya Feisal Salum Abdallah aliyeuzwa Azam FC mapema mwezi huu.
Kisinda pia anakuwa mtu wa tatu kuondoka Yanga kutoka kikosi kilichofika Fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya Kocha Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post