CAF YABADILI MFUMO MICHUANO YA KLABU AFRIKA


SHIRIKISHO la Soka Afrika limeamua kuyatenganisha mashindano yake ya ngazi ya klabu na kuanzia msimu ujao hakuna timu itakayodondokea kwenye Kombe la Shirikisho kutoka Ligi ya Mabingwa.
Kamati ya Utendaji ya CAF katika kikao chake cha leo mjini Rabat nchini Morocco imeamua hakutakuwa na mechi za Raundi ya Pili ya nyongeza ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
Timu 16 zitakazofuzu Raundi ya Pili ya mchujo zitakwenda moja kwa moja Hatua ya makundi kote, kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho na zitakazotolewa safari yao itaishia hapo.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post