ARSENAL YAANZA VIBAYA ENGLAND, YAPIGWA 2-0 NA BRENTFORD

ARSENAL imeanza vibaya Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa 2-0 na Brentford FC usiku huu Uwanja wa Brentford Community, Middlesex.
Mabao yaliyoizamisha Arsenal leo yamefungwa na Mspaniola Sergi Canós dakika ya 22 na kiungo mwenzake, Mdenmark Christian Nørgaard dakika ya 73 wakiipa mwanzo mzuri timu hiyo ya London Magharibi ikicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu baada ya miaka 74.



Post a Comment (0)
Previous Post Next Post