YANGA SC YAMUUZA TUISILA KISINDA ‘BEI YA KUTUPA’ RS BERKANE YA MOROCCO BAADA YA MSIMU MMOJA TANGU IMSAJILI KUTOKA AS VITA

WINGA wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tuisila Kisinda amejiunga na klabu ya RS Berkane ya Morocco kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam.
Kisinda amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu ya Botola Pro  baada ya kukamilisha uhamisho wa dola za Kimarekani 150,000 tu kutoka timu ya Jangwani aliyojiunga mwaka jana kutoka AS Vita ya kwao, DRC.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anakwenda kukutana tena na kocha, Florent Ibenge ambaye ni Mkongo pia waliyekuwa naye AS Vita.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post