HATIMAYE SIMBA SC YAMTAMBULISHA KIUNGO FUNDI WA KIMATAIFA WA MALI, SADIO KANOUTE ALIYEKUWA ANACHEZA LIBYA

 SIMBA SC imemtambulisha rasmi kiungo wa kimafaifa wa Mali, Sadio Kanoute kutoka klabu ya Al-Ahli Benghazi ya Libya.
Kiungo huyo wa zamani wa Stade Malien ya kwao, anakuwa mchezaji mpya wa tisa Simba SC kuelekea msimu ujao.
Wengine ni mabeki Israel Patrick Mwenda kutoka KMC, Mkongo Henoc Inonga Baka kutoka DC Motema Pembe, viungo Jimson Steven Mwanuke kutoka Gwambina FC na Abdulsamad Kassim Ali ' Guti' kutoka Kagera Sugar ya Bukoba.


Wengine ni viungo pia Msenegal Papa Ousmane Sakho kutoka Teungueth Rufisque, Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar, Wamalawi, Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet, Duncan Nyoni kutoka Silver Strikers na wote wapo kambini Jijini Rabat nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya.
Ikumbukee msimu ujao Simba itawakosa nyota wake wawili walioibeba timu kwa misimu miwili iliyopita, winga wa Msumbiji Luis Miquissone aliyeuzwa Al Ahly ya Misri na kiungo Mzambia, Clatous Chama aliyeuzwa RSB Berkane ya Morocco.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post