KIM POULSEN AMREJESHA TAIFA STARS KIPA RAMADHAN KAWBILI WA YANGA KWA AJILI YA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA


KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amemrejesha kikosini kipa Ramadhani Kabwili wa Yanga katika kikosi kitakachoingia kambini Agosti 24 kujiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
Taifa Stars itamenyana na DRC Septemba 2 Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kurejea Dar es Salaam  Septemba 7 kumenyana na Madagascar na Oktoba 10 itaifuata Benin kukamailisha mechi za mzunguko wa kwanza wa kundi lake.



Post a Comment (0)
Previous Post Next Post