KLABUA ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa beki wa kati Mfaransa, Raphael Varane kwa ada ya dola za Kimarekani Milioni 56 kutoka Real Madrid akisaini mkataba wa miaka minne.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Real Madrid mwaka 2011 kutoka Lens ya kwao na katika misimu 10 ameiwezesha klabu kushinda mataji 18, ikiwemo manne ya Champions League na pia alikuwa mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018.
Varane alitambulishwa kwa mashabiki jana Old Trafford kabla ya mchezo wao wa kwanza wa timu hiyo wa Ligi Kuu ya England ikiibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya Leeds United.

Uhamisho huo unakuja wiki mbili baada ya United kumsajili winga wa kimataifa wa England, Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 21 kwa da ya dola za Kimarekani Milioni 100 kutoka Borussia Dortmund.