MMAREKANI CELEB DRESSEL ASHINDA MEDALI YA NNE TOKYO

MMAREKANI Caleb Dressel ameshinda mita 50 freestyle kwenye fainali mapema leo akiweka rekodi mpya kwenye Olimpiki inayoendelea Jijini Tokyo, Japan baada ya kutumia muda wa sekunde 21.07.
Hiyo inakuwa Medali ya nne kwake kwenye Michezo ya Tokyo – na bado ana nafasi ya kushinda moja zaidi kwenye relay.
Florent Manaudou wa Ufaransa amechukua Fedha kwa kumaliza ndani ya sekunde 21.55, wakati Mbrazil, Bruno Fratus ameshinda Shaba akitumia muda wa sekunde 21.57.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post