YANGA SC KUMENYANA NA ZANACO JUMAPILI DAR



VIGOGO, Yanga SC watamenyana na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam 
Siku hiyo pia mwanamuziki nguli barani Afrika, Koffi Olomide atatumbuisha kwenye tamasha hilo maalum kwa Yanga kuzindua rasmi msimu mpya kwa kutangaza kikosi chake pamoja na jezi itakazotumia nyumbani na ugenini msimu ujao..
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Suma Mwaitenda alisema jana pamoja na Koffi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watakuwepo wasanii wengine mbalimbali wa nyumbani.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post