KLABU ya Yanga jana imesaini mkataba wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali na KCCA ya Uganda – hao wakiwa washirika wa tatu baada ya Sevilla ya Hispania na Raja Casablanca ya Morocco.
Yanga inaondoka leo kwenda Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29.
Yanga inaondoka baada ya kutambulisha wachezaji wapya tisa, makipa wapya, Eric Johola kutoka Aigle Noir ya Burundi, Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali, beki wa kushoto, David Bryson kutoka KMC na beki wa kulia Djuma Shabani AS Vita ya kwao, DRC.
Wengine ni winga wa kulia, Jesus Moloko kutoka AS Vita pia, winga wa kushoto, Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC, washambuliaji Yussuf Athumani Biashara United, Fiston Mayele kutoka AS Vita na Heritier Makambo Horoya ya Guinea.