YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA BILA KUFUNGANA NA ATLABARA YA SUDAN KUSINI MECHI YA KUNDI A KOMBE LA KAGAME

 WENYEJI, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 0-0 na Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Sare hiyo ya pili mfululizo baada ya ile ya 1-1 na Nyasa Big Bullet ya Malawi inaifanya Yanga ifikishe pointi mbili tu na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Express ya Uganda yenye pointi sita ambayo imeshatinga Nusu Fainali.
Atlataba na Nyasa Big Bullet iliyofungwa 1-0 na Express leo zinafuatia kila moja ikiwa na pointi moja kuelekea mechi za mwisho.


Yanga itamaliza na Express, wakati Nyasa itacheza na Atlabara katika mechi za mwisho Jumamosi.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post