ENGLAND YAENDELEZA UBABE KUFUZU EURO 2024


MABAO ya Harry Kane dakika ya 37 na Bukayo Saka dakika ya 40 yameipa England ushindi wa 2-0 dhidi ya Ukraine katika mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2024 leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
England inafikisha pointi sita baada ya ushindi wa leo na kuendelea kuongoza Kundi kwa pointi zake sita za mechi mbili, ikifuatiwa na Macedonia Kaskazini pointi tatu, wakati Malta, Italia na Ukraine hazina pointi baada ya wote kucheza mechi moja moja.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post