JKT TANZANIA YAICHAPA TRANSIT CAMP 1-0


TIMU ya JKT Tanzania imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Championship baada ya kuichapa Transit Camp bao 1-0 leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, JKT inafikisha pointi 56 na kuendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi saba zaidi ya Kitayosce baada ya wote kucheza mechi 23, wakati Pamba SC yenye pointi 47 za mechi 22 ni ya tatu.





Post a Comment (0)
Previous Post Next Post