WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana leo amekabidhi Bendera ya Taifa kwa Nahodha Timu ya Fountain Gate, Beatrice Charles inayokwenda nchini Afrika Kusini kwenye Mashindano ya Afrika ya Soka la Wanawake kwa Shule za Sekondari.
Mashindano ya yanatarajiwa kufanyika Mwezi Aprili, 2023 na Fountain Gate ndiyo wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki na Kati - CECAFA katika michuano hiyo.