BALEKE MCHEZAJI BORA LIGI KUU MACHI, ROBERTINHO KOCHA BORA


MSHAMBULIAJI Mkongo wa Simba SC, Jean Baleke ameshinda tuzo ya Mchezajo Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi Machi, huku kocha wake, Mbrazil Robert Oliveira ‘Robertinho’ akibeba tuzo ya Kocha Bora.
Baleke ameshinda tuzo hiyo akiwaangusha Daruwesh Saliboko wa KMC na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons alioingia nao fainali, wakati Robertinho amewashinda Mtunisia wa Yanga, Nasredine Nabi na Abdallah Mohamed ‘Bares’ wa Tanzania Prisons.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post