FOUNTAIN GATE YATINGA FAINALI MICHUANO YA CAF


TIMU ya Fountain Gate ya Dodoma imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya shule za sekondari Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya SCG De Mfilou ya Kongo leo Uwanja wa King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Winfrida Hubert matatu na Mary Siame moja.
Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo kwa upande wa wasichana na wavulana atazawadiwa dola za Kimarekani 300,000 kila mmoja na washindi wa pili watapata dola 200,000 wakati wa tatu atapata dola 150,000.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post