JOSHUA AMSHINDA MMAREKANI KWA POINTI, AMTAKA FURY


BONDIA Muingereza, Anthony Joshua (kulia) usiku wa Jana amefanikiwa kumshinda kwa pointi Mmarekani, Jermaine Franklin katika pambano la uzito wa juu ngumi za kulipwa ukumbi wa O2 Arena, Greenwich kuzipiga.
Pamoja na ushindi huo, lakini hakuwa AJ yule ambaye walimzoea kumuona kwa ubora wa hali ya juu ulingoni kabla ya kupoteza mapambano mawili mfululizo mbele ya Olexsandr Usyk wa Ukraine na kuvuliwa mataji yake ya IBF, IBO, WBA na WBO.
Baada ya pambano hilo Anthony Joshua alisema anamtaka Muingereza mwenzake na bingwa wa WBC, Tyson Fury.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post