MAN CITY YAIBAMIZA LIVERPOOL 4-1 ETIHAD


WENYEJI, Manchester City wameitandika Liverpool mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Alvarez dakika ya 27, Kevin De Bruyne dakika ya 46, Ilkay Gundogan dakika ya 53 na Jack Grealish dakika ya 74, wakati la Liverpool limefungwa na Mohamed Salah dakika ya 17.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 61 katika mchezo wa 27, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na Arsenal ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
Kwa upande wao Liverpool baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 42 za mechi 26 nafasi ya sita.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post