MAYELE APEWA JEZI YA HESHIMA YA MABAO 50 YANGA


WACHEZAJI wa Yanga SC leo wamemkabidhi mwenzao, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele jezi ya idadi ya mabao aliyofunga hadi sasa, 50 zoezi ambalo limefanyika kambini kwao Uwanja wa Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Na imekuwa siku moja kabla ya mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria kesho Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo utakaoanza Saa 2:00 usiku Yanga inahitaji hata sare ili kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Nigeria.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post