ASEC MIMOSA YABANWA NYUMBANI, 0-0 NA USM ALGER


WENYEJI, ASEC Mimosa wamelazimishwa sare ya bila kufungana na USM Alger
katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa jana Uwanja wa Bouaké, Bouaké nchini Ivory Coast.
Timu hizo zitarudiana Mei 17 Uwanja wa Julai 5 1962 Jijini Algiers na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Yanga ya Tanzania na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
Mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Yanga ilishinda 2-0 bila Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam na sasa zitarudiana Mei 17 Afrika Kusini. Fainali zitapigwa Mei 28 na Juni 3 nyumbani na ugenini pia.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post