TANZANIA PRISONS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KAITABA


BAO pekee la Edwin Barua dakika ya 83 limeipa Tanzania Prisons ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 34 na kusogea nafasi ya nane, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 35 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 28.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post