USM ALGER WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


TIMU ya USM Alger imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast usiku wa Jumatano Uwanja wa 
Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
Mabao ya USM Alger yamefungwa na washambuliaji wazawa, Khaled Bovusseliou dakika ya 28 na Abdelfetah Ismaïl Belkacemi dakika ya 80.
Sasa USM Alger watakutana na Yanga iliyoitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini.
Mechi ya Kwanza ya Fainali itachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Mei 28 na marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post