MAYELE MCHEZAJI BORA NA MFUNGAJI BORA MWENZA LIGI KUU


MSHAMBULIAJI Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2022-2023 katika sherehe zilizofanyika usiku wa jana Jijini Tanga.
Ulikuwa usiku mzuri kwa mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga ambayo imebeba tuzo nyingine ikiwemo Mayele kuchukua pia ya Ufungaji Bora kwa pamoja na kiungo Mrundi wa Simba, Saido Ntibanzokiza baada ya wote kumaliza na mabao 17.
Jumla Mayele ameondoka na Tuzo tatu, pamoja na ya Bao Bora la msimu kutokana na bao lake alilofunga kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.
Nyota wa Mali, Djigui Diarra ameshinda Tuzo ya Kipa Bora, Dickson Job Beki Bora na Clement Mzize Mchezaji Bora Chipukizi chini ya umri wa miaka 20 na Mtunisia, Nasredeen Nabi Kocha Bora.
Tuzo nyingine Ntibanzokiza ameshinda pia Mchezo wa Kiungwana na kuwa Kiungo Bora, Mchezaji Bora Chipukizi ni Lameck Lawi wa Coastal Union ya Tanga, KMC timu yenye Nidhamu, 
Upande wa Tuzo za Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Kipa Bora ni Djigui Diarra pia na Mchezaji Bora ni Nahodha wa Yanga, beki Bakari Nondo Mwamnyeto.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post