SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL


KOCHA wa Senegal, Aliou Cissé  amemjumuisha kwenye kikosi chake winga wa Simba SC, Pape Ousmane Sakho kwa ajili ya mbili mwezi huu dhidi ya Benín Juni 17 na Brazil Juni 20 zote ugenini.
Mechi dhidi ya Benín ni ya Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani ambazo wao Ivory Coast ndio wenyeji.
Senegal imekwishajihakikishia tiketi ya AFCON ya mwakani ikiwa inaongoza Kundi L kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Msumbiji pointi nne, Rwanda tatu na Benín mbili kuelekea mechi mbili za mwisho.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post