KIUNGO wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Yanick Litombo Bangala amejiunga na klabu ya Azam FC kutoka Yanga, zote za Dar es Salaam.
Taarifa ya Azam FC leo imesema; “Tumefikia makubaliano na klabu ya Yanga ya kumnunua, mchezaji kiraka, Bangala na amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu vipimo vya afya,”.
