MSHAMBULIAJI chipukizi Mtanzania, Bernard Kamungo Alfajiri ya leo ameifungia timu yake, FC Daollas bao dakika ya 45 katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi kabla ya kutolewa kwa penalti 5-3 na Inter Miami ya Lionel Messi kufuatia sare ya 4-4 Uwanja wa Toyota mjini Frisco, Texas, Marekani.