TWIGA STARS YACHAPWA 2-0 NA IVORY COAST KUFUZU WAFCON


TIMU ya Taifa ya wanawake Twiga Stars jana imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Ivory Coast 
Uwanja wa Yamoussoukro katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) mwakani nchini Morocco.
Timu hizo zitarudiana Septemba 26 Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Djibouti na Togo katika hatua ya mwisho ya mchujo mwezi ujao.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post