KINDA WA AZAM FC KACHWELE AJIUNGA NA VANCOUVER WHITECAPS


CHIPUKIZI wa Azam FC, Cyprian Kachwele amejiunga na klabu ya Vancouver Whitecaps ya Cañada inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
Azam FC imetoa taarifa rasmi ya kumuaga na kumtakia kila la heri katika maisha mapya Vancouver Whitecaps inayofundishwa na Kocha Mtaliano, Vanni Sartini.
“Tunamtakia kila la kheri mshambuliaji wetu chipukizi, Cyprian Kachwele, aliyejiunga na timu yake mpya ya Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS),” imesema Taarifa ya Azam FC.
Kachwele aliibukia akademi ya Azam FC, kabla ya kupandishwa timu kubwa mwishoni mwa msimu uliopita na kucheza baadhi ya mechi, akifunga mabao matatu katika mechi za mashindano.
Anakuwa Mtanzania wa pili Kihistoria kucheza Vancouver Whitecaps baada ya kiungo Nizar Khalfan aliyecheza kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 kabla ya kurejea nyumbani kumalizia soka yake ya Yanga na sasa ni Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post