CHELSEA YAICHAPA CRYSTAL PALACE 2-1 STAMFORD BRIDGE


WENYEJI, Chelsea FC jana wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na MykhailoMudryk dakika ya 13 na Non Madueke kwa penalti dakika ya 89, wakati bao pekee la Crystal Palace lilifungwa na Michael Olise dakika y 45.
Kwa ushindi huo. Chelsea wanafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya 10, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 18 nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 19.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post