KIPRE JUNIOR MCHEZAJI BORA, BRUNO KOCHA BORA LIGI KUU DESEMBA


WINGA wa Azam FC, Zenón Kipre Emmanuel Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Desemba 2023 akiwashinda Prince Dube Mpumelelo anayecheza naye timu moja na Mburkinabe, Stephane Aziz Ki wa Yanga.
Pamoja naye, Kocha wa timu hiyo, Mfaransa Bruno Ferry ameshinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi huo dhidi ya Muargentina Miguel Gamondi wa Yanga na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons.



Post a Comment (0)
Previous Post Next Post