SIMBA SC YASAJILI KIUNGO FUNDI KUTOKA JKU YA ZANZÍBAR


KLABU ya Simba, imemtambulisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Saleh Karabaka kuwa mchezaji wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka JKU ya kwao, Zanzibar.
Saleh Karabaka anakuwa mchezaji mpya wa kwanza Simba SC dirisha hili dogo la usajili na wa kwa ujumla wa kwanza kusajiliwa chini ya kocha Mualgeria, Abdelhak Benchika.
Mchezaji huyo ametambulishwa muda mfupi kabla ya timu hiyo kucheza JKU katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi leo Saa 2:15 usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post