YANGA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI MUIVORY COAST ALIKUWA ANACHEZA UTURUKI


KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Guédé Gnadou (29) kuwa mchezaji wake mpya baada ya kumaliza mkataba wake, Tuzlaspor ya Uturuki.
Guédé anakuwa mchezaji mpya wa tatu Yanga katika dirisha hili dogo, baada ya kiungo Shekhan Ibrahim Khamis (18) kutoka JKU ya Zanzíbar na winga, Augustine Okrah kutoka Bechem United ya kwao, Ghana.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post