CAMEROON YAPANGWA NA BURKINA FASO, ETHIOPIA NA CAPE VERDE AFCON

WENYEJI, Cameroon wamepangwa na Burkina Faso, Ethiopia na Cape Verde katika Kundi A Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitazofanyika Januaari mwakani.
Katika droo iliyopangwa jana, mabingwa watetezi Algeria wamepangwa Kundi E pamoja na Ivory Coast, Equatorial Guinea na Sierra Leone.
Kundi B wapo Zimbabwa, Guinea, Malawi na Senegal, wakati Kundi C wapo Comoro, Gabon, Ghana na Morocco na Kundi D kuna Guinea Bisau, Misri, Sudan na Nigeria na Kundi F zipo Mauritania, Gambia, Mali na Tunisia.


Michuano hiyo itaanza Januari 9 kwa wenyeji, Cameroon kucheza na Burkina Faso.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post