CHIPUKIZI WA AZAM FC MSHINDI WA CECAFA CHALLENGE U23 ATUA UTURUKI KUFANYA MAJARIBIO YA KUCHEZA SOKA YA KULIPWA

CHIPUKIZI wa timu ya vijana ya Azam FC, Paacal Msindo amewasili salama Jijini Antalya nchini Uturuki kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na timu ya Antalyaspor.
Mchezaji huyo aliyekuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, CECAFA Challenge U23 anatarajiwa kuanza majaribio yake Jumatatu.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post