MWANARIADHA WA BELARUS AJISALIMISHA UBALOZI WA POLAND TOKYO

MWANARIADHA wa Belarus, Krystsina Tsimanouskaya ameonekana ubalozi wa Poland Jijini Tokyo leo ambako amejisalimisha kuepuka kurudishwa kwao kufuatia kuingia kwenye mgogoro na viongozi wa timu yake ya Olimpiki.
Serikali ya Japan imesema Tsimanouskaya yu salama baada ya kulalamika viongozi wa timu yake ya Olimpiki walimpeleka Uwanja wa Ndege wa Haneda Jijini Tokyo ili kumrejesha nyumbani Jumapili jioni baada ya kutofautiana na makocha.  
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan amesema wanawasiliana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki nan a Waandaji, Jiji la Tokyo juu ya kumsaidia mwanamichezo huyo.


Krystsina aliwashutumu makocha wa Belarus kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba walimlazimisha kukimbia 4x400 relay licha ya kwamba hakuwahi kukimbia kabla. 
Krystsina ambaye leo anatarajiwa kukimbia mbio za mita 200, amesema anahofia usalama wake akirejea Belarus na ataomba msaada wa Ubalozi wa Austria Jijini Tokyo.  
Krystsina alikimbia mbio za mita 100 Ijumaa na kumaliza nafasi ya nne, ambazo alishinda Mnigeria, Blessing Okagbare, ambaye siku moja baadaye alisimamishwa baada ya vipimo kuonyesha mushkeli kwenye hormone zake. 


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post