SIMBA NA YANGA KUKUTANA SEPTEMBA 25, MWAKA HUU KATIKA MECHI YA NGAO YA JAMII UWANJA WA MKAPA


MECHI ya Ngao ya Jamii kuashiria upenuzi wa pazia la msimu mpya wa 2021/2022 itachezwa Septemba 25, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga.
Mechi ya Ngao ya Jamii hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na wa Kombe la Shirikisho la Soka nchini (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), mataji ambayo yote yalichukuliwa na Simba msimu uliopita.
Lakini kwa sababu Yanga waliomaliza nafasi ya pili Ligi Kuu ndio walicheza na Simba fainali ya ASFC Julai 25 na kufungwa 1-0 mjini Kigoma ndio maana watawania Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post