BEKI WA TAIFA STARS AFCON 2019 AFARIKI DUNIA


BEKI wa zamani wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania, Ally Abdulkarim Mtoni ‘Sonso’ amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mtoni alisajukiwa Yanga akitokea Lipuli ya Iringa msimu wa 2019-2020 kabla ya kuachwa baada ya kuachwa msimu uliofuata akaenda Kagera Sugar ambako aliichezea hadi msimu huu alipojiunga na Ruvu Shooting.
Ally Sonso alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri mwaka 2019.
Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Mtoni Sonso. Amin.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post