YANGA SC YAENDELEZA REKOD YA KUTOPOTEZA MECHI LIGI KUU


MABINGWA, Yanga wameendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.  
Mshambuliaji Mkongo, Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 40, kabla ya kiungo Mganda, Joseph Ssemunju kuisawazishia Mbeya City kwa penalti dakika ya 50 kufuatia Nahodha, Bakari Mwamnyeto kuunawa mpira kwenye boksi.
Yanga wanafikisha mechi 29 bila kupoteza mechi, wakiwa tayari mabingwa kwa pointi zao 73, nyuma yao wakiwa mabingwa wa misimu minne iliyopita, Simba SC wenye pointi 60 za mechi 28 na kesho watamenyana na Tanzania Prisons hapo hapo Sokoine, Mbeya.
Kwa Mbeya City, sare hiyo inawafanya wafikishe pointi 


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post