MANCHESTER UNITED WATINGA FAINALI KOMBE LA FA


TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA Cup England baada ya ushindi wa penalti 7-6 kufuatia sare ya 0-0 na Brighton & Hove Albion FC usiku wa Jumapili Uwanja wa Wembley Jijini London. 
Ni Victor Lindelof aliyefunga penalti ya ushindi baada ya Solly March kukosa upande wa Brighton na sasa kikosi cha Erik ten Hag kitakutana na mahasimu, Manchester City katika Fainali Juni 3 hapo hapo Wembley.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post