KOMBE LA CAF LILILOTUA DAR NA KUONDOKA MWAKA 1993


KOMBE la CAF likiwa mezani Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam Novemba 27, mwaka 1993 kabla ya mchezo wa marudiano wa Fainali baina ya wenyeji, Simba SC na Stella Adjame ya Ivory Coast, ambayo ilishinda 2-0 na kutwaa taji hilo baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Abidjan Novemba 14.
Michuano hiyo ilikuwa inafanyika kwa mara ya pili tu tangu ianzishwe mwaka 1992, 
Uga  Shooting Stars ya Nigeria ikiwa bingwa wa kwanza baada ya kuifunga SC Villa ya Uganda mabao 3-0 katika mechi ya marudiano, kufuatia sare ya 0-0 Kampala.
Mwaka huo, 1992 Tanzania iliwakilishwa na Small Simba katika Kombe la CAF, ambayo licha ya kuwa mshindi wa nne kwenye Ligi ya Muungano 1991 ilinufaika na kufungiwa kwa washindi wa tatu, Simba SC kufuatia kugomea mechi na mabingwa wa mwaka huo, Yanga baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza Uwanja wa Taifa hawakurudi uwanjani kumalizia mchezo.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post