SIMBA SC YAACHANA KIUNGO MNIGERIA VÍCTOR AKPAN


KLABU ya Simba imeachana na kiungo wake Mnigeria, Victor Akpan baada ya msimu mmoja tangu imeshika kutoka Coastal Unión ya Tanga.
Akpan amecheza Simba kwa nusu msimu tu, kabla ya dirisha dogo kutolewa kwa mkopo Ihefu SC ya Mbarali mkoani Mbeya na anakuwa mchezaji wa pili kuruhusiwa baada ya winga Mghana, Augustine Okrah.
“Baada ya kuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu mmoja, Victor Akpan hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao,” imesema taarifa ya Simba mchana huu.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post