MKENYA NDIYE MENEJA MPYA WA SIMBA SC


KLABU ya Simba imemtambulisha Mkenya, Mikael Igendia kuwa Meneja wake mpya wa timu na Mkuu wa Sayansi ya Michezo kwa mkataba wa miaka miwili.
Igendia (36) anachukua nafasi ya Patrick Rweyemamu ambaye amekuwa Mkuu wa Programu za soka la vijana.
Igendia amewahi kufanya kazi na Gormahia FC, timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Uwepo wa Igendia kwenye kikosi ni sehemu ya kuliboresha benchi lake la ufundi kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023/24.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post