COASTAL UNION YAICHAPA MASHUJAA FC 2-0 MKWAKWANI


TIMU ya Coastal Unión ya Tanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Coastal Unión yamefungwa na Bakari Suleiman dakika ya 19 na Lucas Kikoti dakika ya 89 kwa penalti na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 12, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake nane nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi saba.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post