PAMBA FC NA POLISI TANZANIA ZASHINDA, BIASHARA YATOA SARE CHAMPIONSHIP


LIGI ya NBC Championship iliendelea jana kwa michezo minne kupigwa viwanja tofauti, Pamba ya Mwanza ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Green Warriors ya Dar es Salaam bao pekee la Frank Mwenga kwa penalty kipindi cha kwanza Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Mechi nyingine za NBC Championship jana Ken Gold iliichapa Pan Africans 4-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Faountain Gate Talents ikalazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na TMA ikaichapa Mbeya Kwanza 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Ikumbukwe juzi Mbeya City ililazimishwa sare ya 1-1 na Cosmopolitan ya Dar es Salaam Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na Polisi Tanzania ikailaza Stand United 2-1 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Ligi ya NBC Championship inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili zaidi, Cocpo na Transit Camp Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Mbuni FC dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Msimamo wa NBC Championship sasa ni TMA kileleni pointi 15, ikifuatiwa na Ken Gold pointi 13, sawa na Mbeya Kwanza na Pamba pointi 11 baada ya wote kucheza mechi sita.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post