GEITA GOLD YAAMBULIA SULUHU KWA TABORA UNITED NYANKUMBU


WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya Nyankumbu mjini Geita.
Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi saba katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16, wakati Tabora United sasa ina pointi 11 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi tisa.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post